174. Ewe Baba, Bwana wangu
1. Ewe Baba, Bwana wangu, nielekeze mwenendo nifuate neno lako hata leo kaa kwangu! Uwe mlinzi na ngao uongoze maisha mpaka nifike kwako!
2. Umenipa na wazazi walio mkono wako, wanifundisha vizuri, hata na wadhamini, walimu na wakuu Baba Mungu naomba nao uwaongoze!
3. Hata ndugu zangu wote umenipa kwa wema, nisaidiane nao siku zote kwa pendo. Utupe kuungana wakubwa tuheshimu kwa maneno mazuri!
4. Ulikuze kundi letu tukae na adabu, tuinue nchi yetu siku zitungojazo! Nao ufalme wako uenezwe na kwetu, uheshimiwe! Amen.
Comments
Post a Comment