172. Nitwae Hivi Nilivyo



1. Nitwae Hivi Nilivyo, umemwaga damu yako, nawe ulivyoniita, Bwana Yesu naja, naja.


2. Hivi nilivyo si langu kujiosha roho yangu. Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, naja, naja.


3. Hivi nilivyo sioni kamwe furaha moyoni. Daima ni mashakani, Bwana Yesu, naja, naja.


4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu. Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu, naja, naja.


5. Nawe hivi utanitwaa, nisithubutu kukawa, n awewe hutanikataa, Bwana Yesu, naja, naja.


6. Hivi nilivyo mapenzi yamenipa njia wazi, hali na mali sisazi, Bwana Yesu, naja, naja.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu