164. Tumekujia Bwana Wetu



1. Tumekujia Bwana wetu kujiweka mkononi mwako, tuwe wako hata milele twakushukuru na twakusifu. Mwokozi wetu, utukubali, utuongoze njia ya mbingu.


2. Twataka kubatizwa leo kwa jina lako, tuwe wakristo. Umetukomboa na sisi ulipokufa pale golgota, na kwamba wewe upo karibu, unasikia kuomba kwetu.


3. Twakupambia mioyo leo, ingia mfalme w autukufu! Utupe sisi nuru yako tuwe mwanga katika dunia. Pokea leo mioyo yetu, tunajitoa kwkao wenyewe.


4. Tunakuomba sasa, Bwana, usitutie majaribuni, utuongoze siku zote, tukufuate wenye imani. Mwisho tufike kwenye enzi kuu, tuipokee taji ya mbingu.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu