163. Mungu Upokee Moyo Wangu
1. Mungu upokee moyo wangu wote, niwe mtoto wako, siku zangu zote. Nikufuate wewe nisikuache tena, nishike siku zote, ulivypotuagiza. Unisaidie mimi, hata kufa kwangu.
2. Msalabani pako, Yesu naanguka, uliyenifia hata mimi pia. Yaondoe makosa yatoweke kabisa, nipate kuwa safi kwa damu yako bora. Unisaidie mimi hata kufa kwangu.
3. Roho mtakatifu, unanipa nguvu; niweze kushinda majaribu yote, naomba; utawale katika moyo wangu, shetani, hata kufa, usinishinde mimi. Unisaidie mimi, hata kufa kwangu.
4. Baba, Mwana Roho uliye mmoja tu, niliye maskini nakuomba sana; unikubali sasa, katika ubatizo, futa makosa yangu kwa maji haya bora. Unisaidie mimi, hata kufa kwangu.
Comments
Post a Comment