162. Bwana, Twakuletea
1. Bwana, twakuletea mtoto huyu, (watu hawa) tukijua amri yako ya mwisho uliyowapa mitume; watu wote wabatizizwe, watakaokuwa wako.
2. Neno hili ni kubwa tulilopewa na Yesu; atakaye kufika katika ufalme wako, hana budi kuzaliwa tena kwa maji na roho.
3. Pokea kondoo wako Mchungaji mwema Bwana Yesu umwongoze mbinguni (waongoze minguni) ndiwe njia na uzima. Umpe kukutegemea(wape kukutegemea) apate kutengemana (wapate kutengemana)
4. Baba, tunakusihi ukubali wimbo wetu, usikie maombi tunayokuomba sasa. Andika jina la mtoto (andika majina yao) katika kitabu chako!
Comments
Post a Comment