160. Maisha ya Duniani



1. Maisha ya duniani ni mafupi, hata siku ni chache; zinapita hima na kutoweka wala hazirudi, zinatokomea.


2. Vivi hivi kila mmoja tunakwenda mbinguni kwake Mungu, mbele ya kiti chake cha hukumu kila mtu atapewa haki yake.


3. Tunakwenda huko sote na waamini waamini waenda bila woga kwani wanaye Bwana wanaingia nchi takatifu.


4. Ee ndugu, twendeni sote kwake Mungu. Ulimwengu wapiti; utaangamia na dhambi zako, usipokubali nawe waangamia.


5. Basi ndugu tujikabidhi kwa Mungu tuwapo bado hai; kwani tukipuuza tutapotea, hatutaepuka hukumu milele.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu