159. Mbinguni, Mbinguni
1. Mbinguni, mbinguni kuna mji mwema. Wapendeza sana, ni wake Mungu.
2. Milango ya mjini ni dhahabu tu, Mungu ndiye jua anaung’aza.
3. Ugonjwa hauko, huko kufa hakuna, wenyeji wa humo ni wa kweli tu;
4. Waimba usiku hata na mchana wakimsifu Bwana Mungu wetu tu.
5. Wote waimbao wana furaha. Wang’azwa na damu ya Bwana Yesu.
6. Vijana sikieni wote kwamba. Twapenndwa na Yesu, Bwana wa mbingu.
7. Twendeni kuingia wote mjini, tupewe uzima na Bwana wetu.
Comments
Post a Comment