158. Liko Pumziko la Mioyo



1. Liko pumziko la mioyo, amka wee unayechoka, unaugua kama mfungwa kwa shida za moyo wako umtazame kondoo wa Mungu atakuchunga kwa furaha. Uache mzigo enenda. Vita nzuri yamalizika, safari yabaki kidogo inayokusumbua mno.


2. Mungu ametuchagulia pumziko lisilo mwisho amelitengeneza kale, mtu hajazaliwa bado, kufa kwa mfurahisha mponya, tupate pa kupumzikia. Aita, anaalika mioyo inayokaa na shida, msikawie, njooni leo! Ingieni pumzikoni!


3. Ninyi mshindwao na mizigo mlemewao na uzito rukeni kimbieni hima, tokeni pangoni mwenu, msienende kwa muinama, mponya anawaambieni; mimi ni pumziko lenu, ninyi wana wote wa Mungu. Popote mwalizwa na shida, kwa Yesu mwanyamaa kimya!


4. Hapo pumzikeni rahani, wasiwasi hatunao. Shikeni neno hili jema; pumzikeni, Yesu yuko! Shikeni mabawa upesi, karukeni kama ndege wakko jamaa wanangoja; furahi moyo, shangilia, patina nao utukuze, uko mwaka wa pumziko!


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu