157. Mjini ni Mbinguni
1. Mjini ni mbinguni kwa Mungu, hakuna mabaya na shida, waongofu wengi wamejaa wanaomsifu Mwana Kondoo mbinguni, mbinguni mjini ni mbinguni kwa Mungu. Mbinguni mbinguni kwa Mungu ndio mji wa kutupendeza.
2. Wateule wengi wa huko wanaoangazwa na Yesu, huko kuna furaha yetu. Jua lake ni la uzima. Mbinguni,………
3. Moyo wangu una furaha ya kwenda mbinguni kwa Mungu, Bwana univute uliko, kiaga chako kitimie! Mbinguni,……….
4. Kitambo kidogo kipite na mimi nifike mbinguni. Bwana wangu Yesu nakuomba; Ukoo wangu wote ufike Mbinguni,………......
Comments
Post a Comment