156. Umejengwa Juu Yerusalemu



1. Umejengwa juu Yerusalemu, ninakutamani. Moyo wangu ukikutamani, wataka kupita milima na mabonde, kuruka kama tai, uache ulimwengu uingie kwako.


2. Siku nzuri ninaingojea, ifike upesi. Niiache dunia niende mbinguni kwa shangwe. Nimrudishie roho Mwokozi Bwanangu, aipokee vema, aipe uzima.


3. Mara moja roho itakwenda kufika mbinguni, ikiacha uzima wa hapa kwa nguvu ya Mungu. Yapelekwa na gari kama Eliya mkuu, malaika waibeba vizuri kwa shangwe.


4. Nikifika kule Paradiso, mwisho huu ni mwema. Roho yangu yajaa furaha, kinywa husifu tu. Wateule huimba nyimbo nzuri nyingi, hawaachi kumsifu Mungu Mwenye enzi.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu