155. Ondokeni! Tunaitwa



1. Ondokeni! Tunaitwa na walinzi wa juu mnarani Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane, yuaja Bwana wa arusi, wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini kwenda kumpokea Bwana!


2. Sayuni anasikia, moyo waruka kwa furaha, yu macho anaondoka. Mponya wake anashuka mbinguni mwenye utukufu, aleta mwanga wa kweli, taji yake yaja na mwana wa MUNGU Hosiana! Twafuata kwenye shangwe tukale karamu yake.


3. Waimbiwa nyimbo nzuri kwa misemo ya watu wote nay a malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako kwenye milango ya malulu tutakuimbia nasi. Furaha kama hii haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba, tunakusifu, Ee, Bwana.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu