154. Ninataka Kuingia
1. Ninataka Kuingia mjini kwa Mungu. Nitashinda, nitakaza mwendo nifike, nikishikwa na shida, nikichoka njiani, Yesu unaniambia. “uningojee!
2. Naitwa na Yesu Kristo enzi mwake. Nakimbia, kukawia hakuna faida, wote wachelewao hawatapata taji. Mimi sitaki kingine ila uzima.
3. Elekeza macho yangu mlango pako. Niongoze, nipe nguvu, ninapochoka. Ninapojaribiwa, ninaposingiziwa, Yesu, unisaidie nisikuache.
4. Mkono unishike nisianguke. Najiona kuwa mnyonge, nguvu I kwako, neno lako, ee Yesu, linanipa uzima. Nikifika, nitaimba, “Umeniponya:!
Comments
Post a Comment