147. Mtakatifu Wewe, Mungu


1. Mtakatifu wewe, Mungu Mwenye enzi, jua likitoka tutakutukuza wee, Mtakatifu wewe wa huruma nyingi, mwenyezi Mungu wa Utatu.


2. Mtakatifu wewe, waliookoka wakusujudia wewe huko daima. Makerubi wote wakuinamia, Mwenyezi Mungu wa Utatu.


3. Mtakatifu wewe, siri wajificha, macho yetu hayawezi kukutazama, wewe peke yako Mtakatifu kweli, Mwenyezi Mungu wa Utatu.


4. Mtakatifu wewe Mungu Mwenye enzi, kazi zako za kusifu kila mahali Mtakatifu wewe wa huruma nyingi, Mwenyezi Mungu wa Utatu. Amen

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu