139. Mungu Atukuzwe Pekee

 


1. Mungu atukuzwe pekee, shukrani zitolewe sababu ya rehema kuu aliyotutwndea. Mungu atupenda sana, kwa sababu hii ametupa kutengemana vema.


2. Twakutukuza Baba Mkuu twakuheshimu sana, sababu ya kutawala zamani hata leo. Nguvu zako haziishi utakayo yatendeka, Muumba wetu ndiwe.


3. Twakutukuza Ee Yesu mwana wa Mungu wetu na Baba mwenye Enzi. Mwanakondoo wa Mungu, sikia tukikuomba Mwaokozi wetu ndiwe.


4. Twakutukuza Ee Roho uliyekuja kwetu. Uwape nguvu wakristo waliokombolewa. Utuokoe shidani. Shetani asitushinde, Mtuliza mioyo ndiwe.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu