136. Njoo kwetu Roho Mwema



1. Njoo kwetu, Roho mwema, Mfariji wetu. Tufundishe ya Mbinguni, tuwe watu wapya. :/ Njoo, Njoo, Njoo, Roho mwema. /:


2. Utufanye waamini wa Yesu Mwokozi. Tukaishi kikundini kanisani mwako. Njoo, Njoo, Njoo….


3. Kwa huruma tubariki, tuishi na wewe, tukatende kila kitu tuongozwe nawe. Njoo, Njoo Njoo….


4. Roho mwema, Mfariji, utupe hekima; Tukiwaza na kutenda, Yote yawe yako. Njoo, Njoo, Njoo…


5. Tudumishe, tuwe na ukweli wako. Tusivutwe na dunia, Tushu’die neema. Njoo, Njoo, Njoo….

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu