135. Bwana Nasikia Kwamba



1. Bwana nasikia kwwamba umebariki wengi, name nakuomba sasa; Nibariki na mimi! Na mimi na mimi, Nibariki na mimi.


2. Nipitie Baba yangu, kweli mimi mkosaji, Baba uingie kwangu, nirehemu na mimi! Na mimi na mimi Nirehemu na mimi.


3. Nipitie, nakuomba, Bwana Yesu, Mwokozi, wakosaji wawaita, unite na mimi! Na mimi na mimi Uniite na mimi.


4. Nipitie Roho mwema kweli mimi sioni, mwenye nguvu ya kuonya, nipe nguvu na mimi! Na mimi Nipe nguvu na mimi.


5. Nipitie Baba yangu, nakuomba kwa bidii, umebariki wengine, nibariki na mimi! Na mimi na mimi nibariki na mimi.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu