129. Twaomba Roho wa Mungu
1. Twaomba: Roho wa Mungu Mfariji wetu mkuu, utupe Baraka. Yesu alipotuaga, kasema: Namtuma Roho wangu kenu.
2. Utuamshe wakosaji kwa kuwa tu kondoo waliopotea. Uokoe ulimwengu, umeharibika, upate kujuta.
3. Roho wa ujuzi mwingi, fundisha Wakristo wampendeze Mungu. Utufundishe kuomba. Kwa Mungu vizuri, tusikiwe naye.
4. Utusaidie sana, tumshinde Shetani na dunia pia. Tusitengwe na mwokozi, yakija mateso, shida na huzuni.
5. Twakuomba uwe nasi tulio wanyonge tukijaribiwa. Mwisho tutakapokufa, tuone furaha baada ya mateso.
Comments
Post a Comment