128. Roho Mtakatifu Uje
1. Roho mtakatifu uje utukalie na sisi, fanya makao kwetu. Utupe nuru ya Mbinguni, uangaze mioyo yetu, tumtumikie Mingu. Uje, lete utukufu na furaha na uzima; haya twatafuta kwako.
2. U chemchem yenye Rehema, unatunywesha Hekima, watufundisha vema, tuje kuwaambia wenzetu wasiojua habari za wokovu. Roho zetu uzifanye, tuyatende mambo mema wewe utukuzwe sana.
3. Umande mzuri wa Mbingu, geuza mioyo yetu yetu, tujaze pendo lako. Tupendane na wenzetu, tuwafanyie mema tu na kweli watu wote. Kwetu uwe upendan; kugombana kuwe mbali, tuwe na amani daima.
4. Ututakase mioyo, utupe nguvu rohoni, ushike mwendo mwema. Tusifuate kiburi, tama mbaya za mwilini na mambo ya dunia. Roho ziongozwe zifikiri mambo yako, mpaka tufikapo kwako.
Comments
Post a Comment