127. Karibu kwangu Roho



1. Karibu kwangu Roho ingia moyoni, uliyeniletea uzima na raha. Roho Mtakatifu wa Baba na wa Mwana ufananaye nao ukae nao.


2. Unafundisha watu kuomba vizuri, wapate kusikiwa na Mungu Mbinguni Unatuombea, hukomi, mpaka Mungu atende mambo yale uliyoyaomba.


3. Wafurahisha moyo, hupendi huzuni;  tukiwa matesoni, unatutuliza. Wazungumza nasi kwa Neno lako tamu, unatia mioyo furaha ya kweli.


4. Unatufanya sisi kuwa usharika;  hutaki tugombane na kuchukiana. Wanaopigana unawapatanisha;  wataka wapendane Wakristo wowote.


5. Uilinde nchi yetu, serikali yetu, tukae na amani duniani humu. Uwape wakubwa, pamoja na wadogo uchaji na akili, wampendeze Mungu.


6. Katika mwendo wetu utupe sisi nguvu, tumshinde mwovu akitujaribu.  Utusaidie, tushike njia yako na mwisho tufe vema tufike kwa Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu